//
you're reading...
Articles

UKOSEFU WA UTU BAINA YA WANANSIASA KENYA

 BARUA HII NI MARUDIO. TANGU IANDIKWE MAMBO YAZIDI KUCHAFUKA

Barua imeandikwa na Dick Kamau

17.07.07

Kila asubuhi niamkapo nasikitika kuyaona mambo yakichafuka hapa nchini. Mwaka wa 2002 Dec 27 mwenyewe nilidhani kwamba sisi wakenya tumeukataa ukabila na kilichobaki nikuinjenga nchi kwa misingi ya kidemokrasia na maendeleo kama majirani wetu wengine hapa Afrika Mashariki.

Lakushangaza nikuona kwamba wengi wao viongozi wanasiasa hawajali umoja wa taifa letu mbali haja yao ni kuchukua nguvu za dola – state power- hata kama njia wanazotumia na kupanga kuzitumia, sana sana, zitaleta vurugu nchini kote.

Ni mshangao kuona na kujua kwamba matamshi makali ya kuchochea ukabila yanaenezwa kupitia vyombo vya habari zenye kumilikiwa na tabaka la Matajiri wasioijali nchi hii na watu wake maskini ambao ni asilimia 99 ya nchi.

Kwangu magazeti ya Kenya haina tofauti kubwa na yale ya Rwanda, pindi tu kabla ya mauaji ya kihalaiki -genocide.

Kila siku magazeti karibu yote, huvuka mpaka kwa kuchochea chuki na mgawanyiko wa kikabila kupitia makala maalum, barua za wasomaji na hotuba za waeneza chuki ya kikabila. Haya yafanyika bila kufunga jicho kwa minajili ya kuwapigia debe wanasiasa wa makabila fulani ili kuuchukua uongozi wa nchi kijanja na kuwateka nyara maskini mara ya tatu.

Hawa ni baina ya wale ambao kwao ni lazima kuunyakua oungozi sasa kwasababu hawana mda wamezeeka na ikiwa hawapati uongozi sasa uzee utawazidi na kuwa wakongwe akilini mwao. Miaka yao duniani imeanza kupiga taa nyekundu.

Ilikujisikia na kuonyesha kila maskini kwamba wao wanaume kabisa kabla ya kuuacha ulimwengu lazima ndoto zao za kuwa marais, mawaziri na wabunge zitimie bila kujali kama baada ya vurugu mwishowe watakuwepo wananchi wanyonge wakuwasifu na kuwaomba misaada ya CDF na marupurupu ya Kericho(6000). Wamezoea kuabudiwa na maskini hoi.

Nchini Kenya matajiri wezi wenye nguvu, wamejifanya kama kwamba wao ni mungu wa maskini. Maskini wengi wakubali kwamba tajiri akichafua hewa, hewa hiyo mbaya bado nitamu kwa maskini. Huu ni utumwa wa akili! Hewa chafu ni hewa chafu! Haijalishi katokea kwanani binadamu!

Bila aibu tabaka tawala linalindana,  kama tulivyoona viongozi wa Narc wakilinda ufisadi wakupindukia uliofanyika nyakati za utawala wa Kanu na unaoendelezwa sasa na baadhi ya wanasiasa wa Narc Kenya. Ukweli wa mambo ni kama kwamba Kanu bado yakalia ikulu!

Nchi yetu imetoka mstarini wa nchi zenye amani duniani na inakoelekea ni kutumbukia baharini yenye mamba. Tendo hilo litazua uchungu mwingi usio kifani kwa maskini.

Wengine wetu maskini walioonewa twasikika tukisema kwamba Mungu hatakubali mauaji kama ya Rwanda – genocide- yatokee Kenya. Sijui kama wewe mmoja wetu.

Matamshi hayo twayatamka, na wakati huo huo maneno hayajatoka kinywani, polisi waua vijana wetu zaidi ya 100. Wengi wao kisiri, kwa mda wa wiki mbili na kudai ati hawa ni wachukiwa wa Mungiki.

Nchini Rwanda majeshi ya Habyarimana mwaka wa 1994 iliwaita wachukiwa wa RPA/RPF ‘Mende au miti mirefu’! Radio na magazeti ziliwahimiza wahutu kuwapondaponda Mende (watusi) na kuikata miti mirefu (watusi).

Humu Kenya, Waziri Michuku asema watu wajitayarishe na mazishi ya kila siku nakuapa kuwamaliza wachukiwa wa Mungiki na wengineo.

Kila wiki, polisi wa Nairobi zaidi ya elfu 4 washindana nani kaua wachukiwa wengi ili wapewe madaraka. Kule Rwanda askari waliahidiwa mashamba na mali ya watusi. Kenya pia makabila fulani yaahidiwa kumiliki mashamba ya babu zao baada ya Kibaki. Wanasiasa wapigia debe serekali ya majimbo wamesikika wakiapa kwamba wakiitawala nchi mwaka ujao hayo mashamba hata yawe madogo aje, yatanyakuliwa kule Rift Valley na Pwani toka mikononi mwa kabila koloni na fisadi na kupewa makabila miliki yaliyo kalia mashamba hayo kabla ya muzungu kuikoloni Kenya. Ukabila na chuki kiasi hiki ni dhibitisho la ukosefu wa utu baina ya wanasiasa wakatili.

Upande mwingine Serekali ya polisi ili kuonyesha nguvu yaamuru hata mazishi ya wachukiwa wa Mungiki yafanywe bila maombi. Kama ilivyofanyika Rwanda, humu Kenya pia jamii na marafiki wa waliouwawa na polisi sasa hawana haki ya kuwaombea kaka na wazazi wao ili mola aziweke roho zao mahali pema kutungojea sisi – twaja muda si muda!

Jamani, serekali hii usisahau inadai kuna uhuru wakuabudu, kutembelea na kuishi popote utakapo nchini! Uhuru huo umetwaliwa na polisi na baadhi ya wanasiasa wasio ruhusu wenzao kufanya mikutano sehemu fulani za upinzani nchini ikiwemo Nairobi.

Ni wazi kwamba maiti zingine hufichwa na polisi hazipatikani hata baada ya kuzibeba kwa magari ya siri ya polisi. Kusema ukweli polisi wana waua vijana wetu baada ya kuwakamata na kuwachukua vichakani na kuwapiga risasi nyingi. Kwa serekali hii Mungiki lazima wafe wote.

Si ajabu kabla ya uchaguzi ujao vijana wa kikuyu watamalizwa ikiwa umoja wa mataifa hautachukua hatua ya kuiadhibu serekali na kumshitaki Michuki kotini la dunia!

Lakini, ole wangu, wanaokaa kwenye umoja wa mataifa ndio hao hao wanaomsifu waziri Michuki akiwaua Mingiki na kumkashifu akizivamia nyumba za magazeti! Hawa pia ndio wale wale mwishowe watarudi nyuma na kumwita Waziri Michuki katili asiyestahili kuwa waziri. Hao dio walimyima Hon Murungaru Kibali cha kutembelea Ulaya. Kwasababu yakibiashara.

Ajabu kubwa ni kwa waumini wote maskini. Bado Mungu yuko tu na haya yatendeka! Huenda maobi yetu hayafiki popote? Mungu wa maskini yupi? Wamatajiri fisadi nani? Bila vitendo kuhakikisha mambo yaenda sawa inavyohitajika ili kuishi maisha ya kibinadamu na yenye haki sawa, maombi hayafai.

Mambo yameenda mrama! Maombi pia yafanywa kikabila na kisiasa Kenya. Na pesa je kwa mhubiri kama wewe wataka Mungu akubariki uwe kiongozi aliyemchagua Mungu? Wahubiri je kwanini wasiwe marais na wabunge?

Si mola amewabariki kwa hali na mali watumishi wake hapa duniani, mbona wasiwe wenye mamlaka juu ya wafuasi wao nchini pia? Si Mungu aliwateua kuwatumikia watu wake? Kwanini wahubiri wawe na mali bila nguvu za dola? Wajiuliza wao.

Mbona sasa mambo tofauti? Si Uhai wa mtu moja ni sawa na ule wa kila mtu yeyote yule? Uhai wa muchukiwa wa Mungiki si ni sawa na ule wamakundi kama Taliban, Sungu sungu na wezi wa mali ya uma kama wale wa Angloleasing, Goldenberg na wezi wanyakuzi wa mashamba makubwa?

Hao wezi matajiri sio tishio la usalama wa nchi? Naomba kujua usalama wanani huharibiwa na maskini? Sio usalama wa tajiri?

Uhai ni uhai na haustahili kuadhiriwa na polisi au mtu mwingine yeyote yule bila hukumu ya haki na ya kisheria kutolewa na mahakama kuu ya nchi.

Wafu hawasemi yaliyotendeka kabla ya kuuawa! Polisi pekee na wauaji wengine hubaki wenye neno ambalo halina wakulikanusha. Polisi wamekua majaji na wawekaji kamba shingoni mwa wachukiwa.

Haileweki hawa wachukiwa huwa wachukiwa na nani mwingine isipokuwa polisi? Ilikudhibitisha mtu ni mchukiwa kawaida yeye hukamatwa na kuhojiwa pakiwa na paredi ya kutambua nani mhusika wa jambo lililotokea. Afisa wa Polisi hawezi akawa yeye ndiye pekee atakaye mtambua mhalifu bila kuwepo na mshahidi wa nje.

Paredi haifanywi kwa wachukiwa wa Mungiki! Tayari huwa wafu!

Waziri Michuki hana haki ya kuwaamru polisi kuwaua wakenya ovyo wengi wao bila hatia, na wenye hatia bila kupewa nafasi ya kujibu mashtaka wanayofanyiwa na dola! Wezi wahali yajuu ndio pia viongozi na pia ndio hutoa amri kuwaua wachukiwa wadogo.

Ni unafki mwingi kuwasikia wanzungu toka ulaya na Marekani wakiwasifu polisi Kenya ati wanafanya nzuri kuwaua Mungiki na wachukiwa wengine bila kuwafikisha mahakamani!

Kwa vyovyote vile hakuna nchi ulaya itakubali polisi wawe wakiwaua wananchi wake ovyo kama wanyama. Lakini mauaji ya wachukiwa yakifanyika Kenya pongezi zatolewa na wamerika na wazungi wa jumuiya ya ulaya.

Mpaka lini wakenya maskini tulale fofo nakupoteza haki zetu ya kuishi bila kuuawa na polisi na wahalifu? Je, wanasiasa wengi wamenyamaza kwa vile sio kabila lao lamatajiri linapigwa risasi usiku na mchana?

Asilimia 99 ya shinda za nchi yetu zilianzilishwa na wanasiasa ambao kunyakua nguvu za dola ndilo lengo lao. Nguvu za dola kwao ni njia pana ya kupora mali ya uma na kufanya wananchi walio wengi wawe kama watumwa nchini mwao. Wakenya wenzangu shida haijui ukabila na imo kwetu jamii nzima ya wakenya maskini popote tulipo. Nchi hii matajiri na wanasiasa wakiuasha moto kwa kuchochea chuki za kikabila utawachoma wao pia.

Kuendelea kuwaunga mkono na kuwaweka madarakani mabweyenye wafisadi, wenye kueneza uchochezi wa kikabila, ni kama tunajiuliza sisi wenyewe kuzisema sala zetu za mwisho! Wengine baina ya wanaotaka urais nchi hii hawalijui lingine ila kuipora nchi uchi bila kujali aishie wapi maskini. Uwakapo moto wa chuki za kikabila Kenya hawa wataondoka pamoja na familia zao kuishi kwingine nje ya nchi. Watarudi kuwatawala na kuwalalia kama kawaida wale wananchi wanyonge watakaobahatika kukiepuka kifo halaiki!

Kabila letu ni la Maskini! Nikabila la Kibera, Korogocho, Lodwar, Muhuroni, Mandera, wajir, Tana River, mpeketoni, Kamirithu, Manjego Mombasa, Voi, Wundanyi, Kano, Kuria, Kahumbini, Kosovo,Bondo, Kaspul, Kitui, Marlal, Kapenguria,Kajiado, Tigania, Othaya, Kinangop, Giakorino Naivasha, DCK Naivasha, Molo, Olenguruone, Koru, Elgon, Busia, Mathare, Kwamurogi Nakuru, Kiamaiko Nairobi, Thika, Gatundu, Misri Limuru na hapo ulipo au alipo nduguyo maskini!.

Kwa malipo duni, sisi ndio wenye kuzifanya kazi za kuvunja mgongo mashambani ya kahawa, chai, makonge, miwa, mashambani ya maua na chakula. Ni sisi wenye kuzifuga kuku, ngombe na mbuzi wenye nyama tamu.

Sisi ndio wenye kubeba mawe na kakoto kwenye majengo makubwa na manyumba manene ya matajiri. Ni sisi tulinjenga Nyayo House na tukaijenga Ikulu inayoshidaniwa.Tulijenga Jela ya Kamiti, Langata, Kondele na zinginezo.

Ni sisi wenye kuzinjenga barabara zinazopitiwa na magari mazuri ya matajiri. Ni sisi madereva wao. Ni sisi wenye kuzinjenga kuta ndefu zizungukazo makaazi ya matajiri. Mbwa wao wanene na wakali twawapa chakula. Twawaandalia chakula matajiri hotelini na nyumbani mwao huku tukiwalea watoto wao wachanga wanaotupenda nakutuona marafiki. Ni sisi walimu wao wakwanza. Nyumbani waishimo matajiri twaamka mapema na kulala usiku wamanane wakisha lala matajiri wetu. Usiku na mchama twayalinda makazi yao matajiri.

Ni watoto wetu wenye kuajiriwa kazi kama za polisi wanaotuua. Ni sisi tunoatoa kodi kubwa kila siku tununuapo sukari, unga, mafuta taa, dawa na nguo ili kuwapa mishahara na marupurupu polisi, marais, mawawaziri, wabunge na viongozi wote. Kodi twailipia ili waishi maisha mazuri wakati wanatutumikia. Na baada ya kustafu, wasipate shida ya matumizi na raha. Yote haya twatimiza na isitoshe viongozi wasema sisi wazembe na hatutaki kufanya kazi twataka zabure!

Yaani sisi wanjenga nchi twadharauliwa. Ajabu ni sisi wenye kupiga kura kuwapa uwezo wanansiasa kutupora na kutudharau. Yote haya hayawezekani bila sisi kushiriki. Ajabu ni kwamba baada ya kazi zote ngumu sisi twabaki maskini walalahoi. Nambari yetu walalahoi ni zaidi ya milioni 27!

Kwa mfano kabila nyanyasa zaidi linamakao kama yale ya Muthaiga, Harligham, Milimani,Langata,Yahya center na kwingineko kama Widsor Lavington na penginepo unapajua hata wewe. Hawa na familia zao wanamiliki kila aina ya biashara kubwa, majengo manene, mashamba makubwa na nguvu za dola.

Watoto wao ni wakubwa jeshini, wizarani na mabalozini. Watoto wao ni wenye kuzisimamia biashara zao kubwa na ndogo. Baada ya vifo za wazazi wao, hawa kawaida hushindania kumiliki nafasi walioacha wazazi wao. Wingine wao sasa hivi wataka kuwa marais ati kwasababu baba zao walishakua marais, mamakamu wa rais, mawaziri, wabunge na matajiri.

Kwakifupi, nikama kwamba maskini kenya hazai kiongozi! Maskini hawana kiwanda cha kisasa cha kuwazaa viongozi! Miaka 43 tangu uhuru upatikane mitambo ya kiwanda chao maskini cha juakali huzalisha tu watumwa wakuwafanyia kazi matajiri fisadi na viongozi walafi.

Kabila hili ni Kabila ndogo fisadi la Matajiri! Mawaziri wengi na baadhi ya wabunge wa mbunge la sasa wamo kwenye kundi hili. Moi pamoja na mafisadi waliokuwa serekalini yake wote pia wako kwenye kundi hili la kabila la Matajiri fisadi.

Pale waishipo matajiri hamna Mungiki, hamna Taliban, hamna sungu sungu au kundi jipya linalo beba Nyundo machoni mwa polisi. Kama abebavyo kisu na rungu Maasai bila kuchukiwa kuwa na nia au mpango wakufanya uhalifu akitumia hizo visu na rungu, kundi la kubeba nyundo halipigwi risasi kwa kubeba silaha hatari. Haki si kwa wote.

Wachukiwa wahalifu au maskuota hawapo waishimo hawa matajiri. Bila shaka kwao matajiri Kenya ni nchi nzuri yenye amani na maendeleo makubwa. Wasema hawa; wale wasio na macho na wazembe ndio hawayaoni maendeleo makubwa yaliyofanyika tangu uhuru upatikane, na hasa tangu Moi aondoke ikulu.

Tusiziseme sala zetu za mwisho! Waziseme wao mafisadi wakati maskini atakapochukua uongozi!

Kuna njia. Maskini wataepuka njanga la umaskini na kuuliwa uvyo na polisi wakitambua kwamba nijukumu lao wenyewe kujitafutia usalama wakudumu kupitia uchaguzi ujao kwa kuwachagua maskini wenzao uongozini wa nchi!

Diposa kikaundwa chama cha mwananchi – ccm, ili kiwe ngazi ya maskini ya kupaa kwenye uongozi wa nchi. CCM ni mbwa wa maskini kwenda mawindoni ya utawala, kwa niamba yao wenyewe na watoto wao.

NJooni tushirikiane ili tuepuke yajayo maovu. Tumeamua Kuishi!

Toa maoni yako kwa mwandishi wa barua hii.

Katibu mkuu wa CCM 

dickkamau@gmail.com

Advertisements

About SG

Secretary general of Chama Cha Mwananchi. This blog www.chamachamwananchi.wordpress.com, is based in Sweden.

Discussion

No comments yet.

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Advertisements
%d bloggers like this: