//
CCM (Manifesto)

ILANI YA CHAMA CHA MWANANCHI – CCM (Manifesto)

UHURU, HAKI, USAWA NA UAMINIFU.

UANACHAMA
CCM ni chama cha wananchi walioonewa na kunyayaswa sio mabweyenye wanyoyaji.

CCM ni chama cha wakenya wote, sio cha kabila au makabila fulani.

CCM si shamba la wanyama, wanachama wake wote ni sawa.

CCM ni ngome ya kondoo na wala nyasi wote. Haikubali masimba, mafisi na mabweha zizini.Mafisadi, wezi, madikteta, watesi na wasaliti wa nchi wote ni marufuku chamani.

Kauli Mbiu.
Mwanzo Mpya.Watu

Wapya Kenya Mpya.

Itikadi – Taa ya CCM ni Ujamaa na democrasia.

1 – CCM itatawala kwa mjibu wa sheria za haki na kanuni za demokrasia.

2- CCM itawapa wananchi wenye umri mdogo wendelevu na wazalendo nafasi ya kupaa uongozini wa nchi.

3 – Daima CCM itapinga udikteta na itapigania katiba Mpya itakayo futa mizizi ya uimla na kusimamia maslahi na haki za Wakenya wote.

4 – Serekali ya CCM itatetea haki zote za binadamu.

5 – CCM itarejesha maridhiano miongoni mwa Wakenya kwa kuunda Tume ya Ukweli, Haki na Maridhiano kuchunguza madhambi yote waliofanyiana Wakenya ili kuomba wasameheane.

6 – Ndoto ya CCM ni kufanya Kenya nchi iliyoendelea kiuchumi.

7 – CCM itakuza uchumi unaomilikiwa na Wakenya sio wageni.

8 – CCM itazingatia maendeleo ya wasio nacho ya kufuta umaskini, maradhi, jaa na upofu wa kiakili, sio maendeleo ya walio nacho, viongozi na matajiri.

9 – CCM itapigania ugavi wa mali ya nchi unaolenga kumtimizia mwananchi mahitaji yake ya lazima, chakula, nyumba, elimu, matibabu, usafiri……

10 – Serikali ya CCM itatoa bila malipo elimu ya msingi, upili, vyuo vya ufundi na taasisi za utafiti kama msingi wa maendeleo yanayotengemea teknolojia.

11 – CCM itawaomba Wakenya waliong’ambo warudi nyumbani wasaidie kunjenya nchi upya bila kupoteza uraia mwingine.

12 – CCM itamaliza wizi wa mali za umma na serikali kwa kuwafunga wote watakaopatikana na ufisadi.

13 – CCM itashitaki mafisadi warudishe pesa walizopora na kuweka nje, na kushitaki katika Mahakama ya Dunia, serikali ya Uingereza ilipe Kenya, Mau Mau na na mashujaa wengine wa uhuru hasara iliyowapatiliza vitani vya uhuru.

14 – CCM itakuza maendeleo katika sehemu zote za nchi.

15 – Chini ya CCM walio nyuma na walio mbele watakuwa sawa. 16 – CCM itahakikisha uchumi unatolea wasio na kazi ajira na wafanyikazi mishahara bora na haki.

17 – CCM italinda maslahi ya wafanyabiashara wadogo kama vile wachuuzi, wapiga viatu rangi, bodaboda, jua kali na kina mama wa sokoni.

18 – CCM itahakikisha wakulima hawapunjwi jasho lao.

19 – CCM itahakikisha mashamba makubwa zaidi yanapunguzwa na yale hayalimwi yanatwaliwa ili yapewe maskuota na wakazi wa miji ya mabanda.

20 – CCM itahakikisha waathirika wa vita vya kikabila wamepewa mashamba na makao.

21 – Serikali ya CCM itarudisha, kuhifadhi na kupanua misitu na kustawisha utalii kwa kujenga barabara za lami mbugani zetu za wanyama.

22 – CCM itaunganisha nchi kwa misingi ya usawa, uzalendo na utaifa.

23 – CCM itaharamisha ukabila na ubaguzi wake.

24 – Serikali ya CCM itagawa kazi, raslimali na wizara kwa mujibu wa sifa, haki na uhitaji badala ya ukabila, ukoo, familia na urafiki.

25 – Serikali ya CCM itahakikisha popote waishipo Wakenya watakuwa sawa na wasioishi katika makazi yao ya jadi hawatabaguliwa tena na serikali kuu, serikali za mitaa na kundi lolote la kisiasa.

26 – Badala ya majimbo, CCM itatetea Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa nchi na serikali moja ya Afrika Mashariki.

27 – CCM itapiga marufuku ubaguzi wowote wa kijinsia.

28 – CCM itakataa ubaguzi wote wa kidini.

29 – CCM itatetea maadili ya uandishi yatakayo fanya vyombo vyetu vya habari viwe vya watu zalendo, endelevu, sahihi na maadui wa ukabila na ufisadi.

30 – Kiswahili ndicho lugha rasmi ya CCM.

31 – CCM itanjenga uhusiano wa kiamani na kirafiki na nchi zote za Afrika na dunia, ambazo hazina ugomvi na Kenya.

Kateni Minyororo ya Utumwa
Vunjeni Nira za Dhuruma
Piganieni Uhuru wa Walionyanyaswa. Kama wewe Mwananchi jiunge na CCM.

Malipo ya uanachama 100 ksh kumi pekee.

Kama upo nchini unaweza kujiunga na CCM kupitia ofici za CCM nchini na pia kwa kumuandikia barua pepe Katibu Mkuu ukiwa unaishi nje ya nchi. Tumia njia hizo kupitia anuani, simu na email za chama. Pia kupitia nafasi hii upo sasa unaweza kutuandikia na tukawasiliana nawe kwa maelezo zaidi au kujibu swali lako.

(Secretary General) – Tel +254 723454063.

Secretariat +254 721201135,

+254202012578,

Head Office, Secretariat; Down Town Towers, 7th floor, Duruma rd. Nairobi.

P.OBOX 9400– 00100 Nairobi Kenya.

Barua pepe – Email chamachamwanachiccm@yahoo.com

KARIBU CCM.

Maadishi haya yanaweza kutumiwa kwa mjibu wa kuendeleza demokrasia.

Tujulishe tu.

Discussion

No comments yet.

Leave a comment